Simon Msuva Atoa Onyo, Amtaja Kipa Mpya Wa Simba

 


🚨 Simon Msuva ametoa onyo kwa timu za Ligi Kuu akisema “Kipa mpya wa Simba, Ayoub Lakred kutoka FAR Rabat ana kiwango bora sana uwanjani.”


Msuva wakati akiwa Wydad Casablanca, aliwahi kukutana mara kadhaa na FAR Rabat na golini alikuwepo Lakred, hivyo anakumbuka kile kipa huyo alikifanya.


“Mara ya mwisho nilikuwa benchi na timu yetu ilifungwa na FAR Rabat bao 1-0, alionyesha kiwango kizuri ni kipa bora na watu wasishangae kama atachukua nafasi haraka Simba, miaka imeenda tangu kipindi hicho ambacho nilikuwa nikicheza Morocco kwa hiyo sijui kwa sasa kama atakuwa na ubora uleule au umeongezeka lakini kijumla anaweza kufanya mambo makubwa kwenye ligi na ana uzoefu wa kimataifa,” alisema.





Be sure to be back again for more updates! August 16, 2023 at 03:37AM
Next Post Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url