Ngoma Afunguka Alichokiona Simba

 


 Kiungo wa Simba, Fabrice Ngoma amesema kwa uzoefu wake na soka la Afrika, Simba ina kikosi kizuri ambacho kinaweza kubeba ubingwa wa ligi na hata Ligi ya Mabingwa Afrika.


RECOMMEND: Soma Hii > YANGA WABWAGA MANYANGA

“Tuna timu nzuri, ushindani ni mkubwa na malengo yetu ni kufanya vizuri na kutwaa mataji. Ligi ni ngumu na inaushindani mkubwa, lakini pia ndani ya timu kuna ushindani wa kutosha kutokana na aina ya wachezaji waliopo kila mmoja ana ubora na sifa zake. Kama wachezaji tumejipanga kufanya vizuri ili kufikia malengo, na naamini tutafanya vizuri zaidi msimu huu na kuwapa furaha mashabiki wa timu hii.”


Kiungo huyo wa zamani wa MK Etancheite na AS Vita za DR Congo, Ifaenyi Ubah ya Nigeria, Raja Casablanca ya Morocco, Al Faheheel na Al Hilal za Sudan aliwahi kutakiwa na mabingwa watetezi wa ligi, Yanga lakini baadae alichagua kujiunga na Simba.





Be sure to be back again for more updates! August 25, 2023 at 05:16AM
Next Post Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url