Robertinho, Kocha Wa Simba Atikisa Kiberti

 


Kocha Wa Simba SC amefunguka mengi mara baada ya kutwaa ngao ya jamii. Mbali na kukiri kuwa katika mchezo huo kipindi cha kwanza hawakufanya vizuri ila alikua na haya ya kusema;


“Haikuwa rahisi lakini nawapongeza wachezaji wangu hii ni mechi ya watani huwa ina ugumu wake lakini kwetu jambo kubwa tumechukua hili taji la kwanza na safari inayofuata ni kuanza kuyasaka mengine,” alisema.

“Unapoanza kuanza msimu na mafanikio kama haya kuna morali kubwa inajengeka kwenye mioyo yetu, nimekuta klabu hii ina miaka miwili bila taji kwa hadhi ya Simba haikuwa sawa sasa tunaingia kwenye ligi tukiwa na nguvu kubwa.

“Mimi ni kocha ambaye kote nilikopita nimekuwa natamani kuchukua mataji na nimekuwa nayapata, bahati mbaya hapa mwaka wa kwanza sikupata kombe lolote na kulikuwa na sababu na huu ni mwanzo.





Be sure to be back again for more updates! August 16, 2023 at 01:50AM
Next Post Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url