Matokeo kidato cha sita 2023



Matokeo kidato cha sita 2023, Fom 6 results, Matokeo Ya Form Six


Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) imetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023 huku yakionyesha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka jana.


Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Julai 13, 2023 katika ofisi za Baraza hilo Zanzibar, Katibu Mtendaji wa Necta Dk Said Mohamed amesema jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani ni 106, 883 huku wasichana wakiwa ni 47, 340 na wavulana 59, 543.


Serikali kuwafadhili watakaosoma Tehama Zanzibar
Kitaifa 33 min ago
"Jumla ya watahiniwa 104,549 sawa na asilimia 99.23 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita 2023 wamefaulu," amesema.

Wasichana waliofaulu ni 46,707 sawa na asilimia 99.51 huku kwa upande wa wavulana, waliofaulu ni 57, 843 sawa na asilimia 99.

Mwaka 2022 waliofaulu walikuwa 93,136 sawa na asilimia 98.97 hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka 2023

Kutazama Matokeo Bonyeza Hapa




Be sure to be back again for more updates! July 13, 2023 at 05:30AM
Next Post Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url